Mahakama Nchini Kenya, imeiondoa kesi ya kupinga uamuzi wa Serikali wa kuruhusu uingizaji na kulima mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki, ili kusaidia kukabiliana na tatizo la chakula.

Hatua hiyo, inafuatia Serikali kuondoa marufuku ya muongo mmoja kwa mazao ya GMO hapo Oktoba 2022, ili kukabiliana na upungufu wa usalama wa chakula kufuatia ukame mbaya uliolikumba eneo la Pembe ya Afrika.

Baadaye, Wakili Paul Mwangi aliwasilisha kesi Mahakamani akidai uamuzi huo ni kinyume cha katiba, kwani kulikuwa na wasiwasi juu ya usalama wa mazao.

Hata hivyo, Oktoba 12, 2023 Hakimu wa Mahakama ya Mazingira, Oscar Angote aliamua kwamba hakuna ushahidi wowote wa unao onesha madhara yoyote ya asili au afya ya Binadamu kutoka kwa mazao hayo.

Mke wa Rais jela kwa utakatishaji fedha, kughushi nyaraka
Serikali yawataka Wafanyabiashara wa Madini kufuata taratibu