Inspekta Mkuu wa zamani wa Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo – DRC, John Numbi amemshambulia Rais Felix Tshisekedi huku akikaribia kutoa wito wa kufanyika mapinduzi nchini humo, kwa madai kadhaa ikiwemo yale ya kumtuhumu Kiongozi huyo wa Nchi kushindwa kumudu Uongozi wa nchi hiyo.

Matamshi ya Inspekta Numbi yanakuja wakati ambapo wagombea urais wamewasilisha nyaraka zao za kutaka kuwania nafasi ya uongozi wa nchi hiyo, katika uchaguzi unaotarajia kufanyika Desemba 2023.

Inspekta Mkuu wa zamani wa Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo – DRC, John Numbi.

Hata hivyo, huenda matamshi yaliyotolewa na Inspekta Numbi hayatishii au ahayatafanyika kama ambavyo amesisitiza, lakini matamshi hayo yanawatia hofu watu walio karibu na wandani wa Rais Tshisekedi ambao wanatajwa kuinamisha vichwa chini kuchukua tahadhari.

Inspekta Mkuu huyo wa zamani, John Numbi, alikuwa na umuhimu mkubwa katika utawala wa rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila ila ushawishi wake ulipungua Kabila alipokabidhi madaraka kwa Felix Tshisekedi.

Kombe la Dunia 2034: Saudi Arabia majaribuni
Mfumuko wa bei wachangia uwepo baa la njaa