Chelsea wamemwongeza mshambuliaji wa SSC Napoli, Victor Osimhen kwenye orodha ya wachezaji wanaowalenga wakati wa dirisha dogo la Januari 2024, kwa mujibu wa ESPN.

Chelsea wanatafuta mshambuliaji wa kati na tayari wanamfuatilia mchezaji wa Brentford Ivan Toney, ambaye pia anavutiwa na Arsenal kama ESPN ilivyoripoti Septemba 26, mwaka huu.

Osimhen amejijengea sifa ya kuwa mmoja wa washambuliaji wa kufurahisha zaidi barani Ulaya baada ya kufunga mabao 26 katika mechi 32 za Ligi Kuu Italia msimu uliopita huku SSC Napoli ikitwaa taji lao la kwanza la Serie A tangu mwaka 1990.

Kiwango hicho kizuri ambacho kimeendelea hadi msimu huu kwa mabao sita kutoka mechi 10 kimepelekea SSC Napoli kuweka dau la Osimhen hadi pauni milioni 120, ambayo ni karibu pauni milioni 40 zaidi ya thamani ya Toney.

Chelsea wanatarajia Christopher Nkunku, aliyesajiliwa kwa dau la Pauni Milioni 52 kutoka RB Leipzig kupatikana mapema mwaka mpya baada ya upasuaji wa goti kwa kuongoza safu ya ushambuliaji pamoja na Nicolas Jackson na Armando Broja.

Young Africans yaihamisha Geita Gold FC
El-Nino: Serikali imetekeleza hatua za awali - Mhagama