Imefahamika kuwa wamiliki Manchester United familia ya Glazers wanapanga kufanya kikao cha bodi kwa ajili ya kujadili uwezekano wa kuipiga bei timu hiyo mara baada ya kuwepo kwa wateja wapya walioonyesha nia ya kutaka  kuinunua.

Ni takriban mwaka mmoja umepita sasa tangu Glazers walipotangaza kuwa wapo kwenye mchakato wa kuuza timu hiyo, huku familia ya Glazer inakabiliwa na maamuzi makubwa kuhusu zabuni zilizosalia kwenye mchanganyiko huo.

Wamiliki wa Manchester United familia ya Glazer wanatazamiwa kufanya mkutano wa bodi ndani ya siku chache kutoka sasa ili kujadili mapendekezo mapya kutoka kwa Sir Jim Ratcliffe, imefahamika.

Bilionea wa Uingereza Ratcliffe na mpinzani wake mzabuni, Sheikh Jassim bin Hamad al Thani wote wamewasilisha zabuni nyingi tangu Glazers ilipotangaza mnamo Novemba 2022 kwamba walikuwa tayari kuiuza klabu hiyo.

Ripoti ya Bloomberg inaonyesha “hakuna uhakika” Glazers watakubaliana na pendekezo jipya la Ratcliffe.

Kuna nafasi pia, Sheikh Jassim kuongeza ombi lake mwenyewe, ingawa benki ya Qatar hadi sasa imeonyesha upendeleo wa kukamilisha umiliki kamili badala ya kuchukua hisa ndogo katika klabu na msemaji wake aliiambia Bloomberg ofa kama hiyo imesalia mezani.

Che Fondoh Malone akabidhiwa Al Ahly
Waasi wa ADF wafanya shambulizi la kifo