Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, linamshikilia mtuhumiwa Expeling Amara Projestus (18), Mmakonde wa Amani kwa kosa la wizi wa kutumia nguo za Wauguzi na kujifanya Muuguzi katika Hospitali ya rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi wa Polisi, Richard Thadei Mchomvu amesema mtuhumiwa huyo alibainika na baadhi ya Wauguzi ambao waligundua kuwa hana sifa na kujihusisha na vitendo vya wizi wa nguo za Wagonjwa Hospitalini hapo.

Aidha, amesema kupitia operesheni mbalimbali tarehe 30/8/2023 katika eneo la Forodhani Zanzibar lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Khelef Khamis Abeid (18), mshirazi wa Bububu Kijichi akiwa na Bastola aina ya Bareta yenye namba 69085 ikiwa na risasi nne ndani ya kisanduku cha kutunzia risasi.

Amesema, baada ya kupekuliwa nyumbani kwake mtuhumiwa huyo alikutwa na risasi moja akiwa ameificha ndani ya nyumba hiyo na kwamba Upelelezi unaendelea na utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Katika Mkoa wa Mjini Magharibi, jumla ya watuhumiwa 53 walimatwa kwa makosa ya unyang’anyi kwa kutumia silaha zikiwemo Simu 58, Kompyuta mpakato, Pikipiki zilizonyanganywa katika maeneo mbalimbali pamoja na mapanga 33 yanayotumika kufanyia uhalifu huo.

Hata hivyo, Kamanda Mchomvu amesema, katika kipindi cha miezi tisa mwaka 2023 jumla ya kesi 20 za udhalilishaji zilipata mafanikio Mahakamani na kuwatia hatiani watuhumiwa kwa kutumikia adhabu za vifungo kuanzia miaka 10 – 30 pamoja na kulipa faini na fidia kwa wahanga.

Rais Samia ahitimisha mbio za Mwenge wa Uhuru Manyara
Ajali yauwa Viongozi sita wa CCM Njombe