Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, John Imori amethibitisha kutokea kwa vifo vya Watu sita ambao ni Viongozi wa Chama cha Mapinduzi -CCM, Kata na UWT Wilayani Makete Mkoani Njombe, vilivyotokea kwa ajali ya gari wakati wakitoka kwenye mkutano wa Mlezi wa CCM Mkoa wa Njombe, Halima Mamuya.

Amesema ajali hiyo iliyotokea Kijiji cha Ndulamo kwa kuhusisha Gari lenye namba T 733 BBP aina ya Toyota Hiace, lililokuwa likitokea Makete kuelekea Tandala, likiwa na abiria 18 ambalo lilipinduka katika kona kutokana na mwendo kasi na kuuwa watu hao sita (Watatu Wanaume na Watatu ni Wanawake).

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Juma Mfanga amesema majeruhi wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Ikonda na wengine wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Makete.

Kufuatia ajali hiyo, Halima Mamuya ametoa pole kwa Familia za marehemu na majeruhi na kuishukuru Serikali kwa hatua za haraka zinazochukuliwa kwa ajili ya matibabu na kusema Waliofariki ni Viongozi wa Chama wawili, Kiongozi wa Jumuiya ya Wazazi mmoja na Viongozi wa Jumuiya ya Wanawake watatu.

Muuguzi mwizi nguo za Wagonjwa aifikia siku ya 40
Njia moja lakini malengo tofauti