Tanzania imeishauri Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF, kukifanya Kiswahili kuwa miongoni wa lugha za mawasiliano wakati wa mikutano yake, kutokana na kukua kwa lugha hiyo na kutumika kwenye mikutano mingine ya Kikanda na Kimataifa.

Ushauri huo, umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, wakati wa Mkutano wa 26 wa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa Benki ya Dunia unaofanyika Mjini Marrakesh nchini Morocco.

Amesema ni wakati muafaka wa kukijumuisha Kiswahili katika mijadala ya Taasisi hizo kubwa za Fedha duniani kwa kuwa wanachama wake wengi kutoka katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, wanazungumza lugha hiyo.

Wakati wa Mkutano wa 27 wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa Benki ya Dunia, wakati wa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), itakayofanyika Washington D.C, nchini Marekani, Aprili, 2024 ajenda hiyo itajadiliwa.

Al Ahly kutua Dar es salaam Oktoba 17
Wahamasishwa kutoa ushahidi kukomesha uhalifu