Rais Samia Suluhu Hassan ameibua hofu kwa Vyama vya upinzani nchini katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao wa 2025, kutokana na umati mkubwa wa watu anaovutia katika ziara zake za mikoani.

Popote aendapo kwenye ziara hizo, Rais Samia amekuwa akilakiwa na umati mkubwa wa watu na kuwafanya wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini kutabiri kuwa huenda Rais Samia akashinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Kada mbalimbali za Wananchi, ikiwemo Madereva Vijana wa bodaboda, Mama Lishe, Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Wafanyabiashara na Wananchi wa kawaida wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kumpokea Rais Samia kwa umati mkubwa.

Ingawa bado ni mapema na Rais Samia mwenyewe hajatangaza hadharani kuwa atagombea urais 2025, lakini anaonekana kwa sasa kuwa ndiye Mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa zaidi katika vyama vyote vya siasa nchini.

Katika ziara zake za hivi karibuni kwenye mikoa ya kusini na sasa katikati ya Tanzania kwenye Mkoa wa Singida, Umati mkubwa wa maelfu ya watu umekuwa ukijaza viwanja vya mipira, mikutano ya hadhara na hata barabarani Rais Samia anaposimama kuwasalimia wananchi.

Alexander Arnold: Sina nafasi maalum uwanjani
Robertinho afichua mbinu za kuifunga Al Ahly