Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Ariziki Makwaya amewataka Wakaguzi wa Jeshi la Polisi Mkoani humo kuzingatia mambo muhimu ya kiafya, ili kuwajenga kimwili na kiakili kwa manufaa ya sasa na baadaye.

Makwaya ameyasema hayo wakati alipokua akitoa somo kwa wakaguzi hao kuhusu Saikolojia na Afya ya Jamii, ambapo alisisitiza kila mmoja kujali afya yake ili aweze kujiepusha na magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika.

Amesema, inatakiwa wazingatie ulaji sahihi wa vyakula kwa kuzingatia mlo kamili, unywaji wa Maji kwa wingi na kupata muda wa kufanya mazoezi, ikiwezekana kwa wiki mara tatu hadi mara tano kwani Afya njema huanzia ndani ya mtu.

Aidha, amesisitiza kuwa pia inatakiwa kuwa na moyo safi wenye kufanya Ibada, Moyo wenye upendo na unaofurahia mafanikio ya mwingine, usio na wivu wala kuweka vitu vibaya ndani yake huku akiwasisitiza kuwa na furaha muda mwingi.

Wananchi jielekezeni kwenye fursa - Rais Dkt. Samia
Mzozo Gaza: Biden aamua kumfuata Netanyahu