Klabu ya Arsenal ina uhakika wa asilimia zaidi ya 70 beki wao kisiki Ben White atasaini mkataba wa kuendelea kusalia kwenye timu yao kwa muda mrefu zaidi.

White ambaye huduma yake inawindwa na baadhi ya timu kubwa barani Ulaya, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026 na yeye mwenyewe anadaiwa kuwa na furaha zaidi ya kuendelea kusalia Arsenal.

Mazungumzo baina ya Arsenal na wawakilishi wa staa huyu yalianza tangu Agosti na Septemba mwaka huu na hadi sasa yamefikia hatua nzuri.

Mabosi wa Arsenal wamewekeza nguvu zao zote kwa White kwa sasa baada ya kumalizana na Martin Odegaard aliyesaini mkataba mpya mwezi uliopita.

Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 12 za michuano yote na kufunga bao moja, huku akiwa mmoja ya mhimili muhimu kwenye eneo la kiungo cha chini.

Mpango wa kumsainisha mkataba mpya White ambaye alitua Arsenal mwaka 2021 akitokea Brighton unatokana na baadhi ya timu ikiwemo Man City kudaiwa kuimendea huduma yake.

Kamati yashauri kutanua wigo fursa za ajira kwa Watanzania
Moses Phiri kujivisha kitanzi Simba SC