Kiungo Mshambuliaji wa Azam FC ambaye ni Raia wa Gambia, Gibril Sillah amesema Simba SC ina heshima kubwa katika mataifa mengine kutokana na miaka ya hivi karibuni kufanya vizuri kwenye mashindano ya klabu Afrika.

Gibril amesema kabla hajasajiliwa Azam FC akiwa na Raja Club Athletic ya Morocco ilikuwa ikitajwa Tanzania na wachezaji wengi walikuwa wanatamani kupata nafasi ya kuitumikia Simba SC kutokana na ushiriki wake katika mashindano hayo.

Ilikuwa ikitajwa Tanzania, wachezaji wa mataifa mengi yalikuwa yanaitazama Simba SC kutokana na kufika hatua ya Robo Fainali mara nyingi, hiyo ilifanya baadhi ya mastaa wao kufuatiliwa kwa ukaribu,” amesema.

“Ndio maana ilikuwa rahisi kuwajua kina Clatous Chama, Luis Miquissone ambao walifanya vizuri kwenye michuano hiyo ukiondoa rafiki yangu Pape Sakho,” alisema mchezaji huyo.

Mbali na Simba SC, Gibril aliitaja Young Africans kuanza kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa baada ya mwaka jana kufika fainali za Kombe la Shirikisho Afrika.

“Kwa sasa Young Africans inaingia kwenye anga za Simba SC ambayo tayari ilijiwekea mizizi yake kwenye michuano ya CAF, hilo linaonyesha namna ambavyo Tanzania inapiga hatua kubwa ya kukua kwa soka,” amesema

“Nimegundua ushindani unaanzia kwenye ligi ya ndani ndio maana timu zinazopata nafasi ya kushiriki michuano ya CAF zinafanya vizuri.”

Sillah amekuwa mmoja kati ya wachezaji tegemeo wa kikosi cha Azam FC ambacho kinashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara kikiwa na pointi 13 baada ya michezo mitano.

Afrika, Nordoc zakubaliana kuboresha Biashara, uwekezaji
Rais Samia azungumza na Wafanyabiashara Nzega