Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Jesse Lingard anakaribia kusaini katika klabu ya Saudia Pro League, AI Ettifaq mara baada ya muda wake wa kutazamwa mwenendo wake kwenda vizuri.

Klabu hiyo inanolewa na nahodha wa zamani wa England na Liverpool, Steven Gerrard imeweka wazi kuwa msimu ujao watakuwa na Lingard baada ya kuridhishwa na maendeleo yake.

Gerrard anataka kumsajili Lingard lakini itabidi asubiri hadi mwezi Januari kutokana na sheria za kusajili wachezaji wa kigeni nchini Saudi Arabia kubana kwa sasa.

Wachezaji wa kigeni Saudi wanapaswa wasizidi 8 kwenye orodha wa wachezaji wanaocheza mechi na mpaka sasa Al Etifaq ina wachezaji 10 wa kigeni.

Kwa mantiki hiyo kuna namna ambavyo klabu hiyo itawatoa baadhi ya wachezaji ili wapitishe jina la Lingard.

Jobe kumfuata kaka yake Real Madrid
Cedric Kaze: Singida BS wameshika ajira yangu