Lydia Mollel – Morogoro.

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, linamshikilia mtu mmoja Rhoda Peter (30), mkazi wa Kihonda kwa tuhuma za kutupa kichakani Watoto wachanga mapacha wenye jinsia ya kike na kiume, wanaokadiriwa kuwa na umri wa siku moja katika eneo la kihonda ndani ya manispaa ya Morogoro.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amesema wamemkamata mwanamke huyo kwa kushirikiana na Wananchi wa eneo hilo na wanamshikilia kwa taratibu mbalimbali za kisheria.

Aidha jeshi hilo pia limemkamata Glory Barnabas (23) mkazi wa wa Tungi kwa kosa la wizi wa mtoto wa kike anaekadiriwa kuwa na umri wa miezi mitatu.

Katika hatua nyingine jeshi hilo linawashikilia watu Sita kwa tuhuma za wizi kwa kutumia Pikipiki huku Kamanda Mkama akitoa wito kwa Wazazi na Walezi kuwalea Vijana katika maadili yanayostahili, ili kuwaepusha na vitendo vya kihalifu.

Cedric Kaze: Singida BS wameshika ajira yangu
Thiery Henry: Huyu Messi ni balaa