Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema migogoro inayoendelea ulimwenguni, imezidi kuimarisha mahusiano Kati ya nchi yake na China huku  huku Rais Xi akisema anatumai Mataifa yao yatafanya kazi pamoja, katika kulinda haki za Kimataifa.

Kauli ya Putin imekuja mara baada ya kufanya mazungumzo na rais wa China, Xi Jinping katika ziara yake ya kwanza kwenye Taifa hilo lenye uchumi mkubwa duniani, tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Vladimir Putin (kushoto) na Xi Jinping.

Putin na Xi walikutana jijini Beijing pembezoni mwa Kongamano la China linalohusu mradi mkubwa wa miundombinu ya barabara na Reli ambapo mazungumzo ya viongozi hao yaligubikwa na mzozo wa Mashariki ya Kati.

Kongamano kuhusu mradi wa China wa Miundombinu ya barabara na reli katika nchi zinazoendelea, pia ulihudhuriwa na wajumbe kutoka zaidi ya nchi 130, wakiwemo Viongozi wa juu wa Serikali.

Polisi kuwasaka waliowauwa Watalii, muongozaji wao
Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 19, 2023