Kocha Msaidizi wa Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars), Esther Chabruma, amesema kikosi hicho kinaendelea kujifua kwa sababu kinahitaji kufanya vizuri katika mechi za mashindano yote zinazowakabili.

Twiga Stars inatarajia kuwakaribisha Botswana katika mechi ya kusaka tiketi ya kucheza Michezo ya Olimpiki itakayochezwa Oktoba 26, mwaka huu na kurudiana baada ya siku tano baadae, huku ikikabiliwa na mchezo mchezo mwingine wa kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON 2024) dhidi ya Togo.

Chabruma amesema kila mechi ni muhimu na kikosi chao kimekuwa katika mazoezi kwa muda mrefu kwa sababu wanahitaji kufikia malengo.

“Mechi zote ni ngumu, tunafanya mazoezi maalum ya kuhakikisha tunapata ushindi katika kila mechi na hatimaye kusonga mbele, tunahitaji kuendelea kuipa heshima bendera ya Tanzania,” amesema kocha huyo ambaye alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Twiga Stars.

Twiga Stars ilisonga mbele katika michuano ya Afrika baada ya kuwaondoa lvory Coast wakati Kenya iliwatupa nje Cameroon na Burundi ikawafunga Ethiopia.

Ángel Di María: Timu ya taifa ndio basi tena
Jude Bellingham anogewa Real Madrid