Wakati kikosi chake kikiendelea na maandalizi ya kuikabili Young Africans, Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo, amesema bado yupo sana katika timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Dabo ametoa kauli hiyo kutokana na baadhi ya mashabiki kudai kocha huyo angetimuliwa mapema katika kikosi hicho.

Kocha huyo raia wa Senegal amesema yeye ni mzoefu katika kazi hiyo na kila siku alikuwa anaamini atafikia malengo yake.

“Sikuwa na wasiwasi, nilijua Oktoba 14, Nyerere Day nitakuwa hapa, na waliposema vile niliwasikia, nilikuwa nacheka tu. Unajua hata wamiliki ilipofika Oktoba 14 walinitumia ujumbe kunikumbusha baadhi ya mashabiki walisema sitafika siku hii.” amesema kocha huyo ambaye kwa sasa kikosi chake kinashika nafasi ya pili katika msimamo Ligi Kuu Tanzania Bara.

Azam FC itavaana na mabingwa watetezi, Young Africans katika mechi ya mzunguko wa sita itakayochezwa Oktoba 22, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.

Mzumbe, eGA wakubaliana huduma za Kitaaluma, Teknolojia
Ángel Di María: Timu ya taifa ndio basi tena