Marafiki wa Wanandoa waliouawa wakiwa kwenye fungate pamoja kiongozi wao katika Mbuga ya Kitaifa ya Queen Elizabeth nchini Uganda, wametoa heshima zao za mwisho za kuaga miili ya marehemu.

Wanandoa hao, David na Celia Barlow kutoka Hampstead Norreys wamewaachia watu simanzi kutokana na shambulio lililofanywa na waasi wa ADF, lililopelekea vifo vyao na Polisi wa Uganda walisema gari lao lilichomwa moto baada ya kuuawa.

hata hivyo, Msimamizi wa Kanisa la St Mary’s la Hampstead Norreys, Richard Davies alisema ni vigumu kukubali taarifa hiyo na kudai kuwa, “tunaamka leo tukiwa na huzuni kubwa, kusikia habari mbaya za kifo cha Dave na Celia Barlow,Maneno hayawezi kueleza jinsi tulivyopokea habari hii ya kutisha” alisema Davies

Baraza la Parokia ya Hampstead Norreys, lilimuelezea Barlow, raia wa Uingereza, kama mwenyekiti wa kipekee ambaye alitumikia baraza hilo kwa zaidi ya muongo mmoja huku taarifa ya kampuni ya usafiri ya Belmond, ikimtaja kama Celia Geyer.

KMC FC yatuma salamu Tabora United
GGML wafanya matembezi uhamasisha mwezi Afya ya akili