Scolastica Msewa, Rufiji – Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge ametembelea Maeneo yenye viashiria vya kutokea athari za Mvua za Elnino huko Muhoro Rufiji na kuwataka Wakazi kuhama maeneo hayo.

Kunenge alitembelea hapo kwa lengo la kukagua baadhi ya maeneo ya Kata ya Muhoro ambapo amefanya ziara hiyo ya Wilayani Rufiji Tarafa ya Muhoro, akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele.

Pia, Mkuu huyo wa Mkoa alipata wasaa wa kuzungumza na Wananchi juu ya madhara yanayoweza kujitokeza na kuwasihi kuchukua tahadhari mapema kwa kufuata ushauri wa Serikali.

Mwaka 2021, eneo hilo liliathirika na Mvua kubwa na Serikal iliwatafutia eneo mbadala Wakazi wa maeneo hayo na kuwagawia Viwanja, huku Wananchi wakiipongeza Serikal kwa kuwapa tahadhari na kukubali kuhama.

Habari ya kushangaza Dodoma
Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 20, 2023