Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo – FAO, Dkt. Qu Dongyu amesema kuwa Shirika hilo limevutiwa na mradi wa kuwawezesha vijana unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania wa Jenga Kesho Iliyobora “Building Better Tomorrow” (BBT).

Majaliwa ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Ofisi za Makao Makuu ya FAO zilizopo Rome, Italia ambapo Majaliwa yuko nchini Italia akimuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani ulioanza Oktoba 16 – 20, 2023.

Amesema, “FAO tutaunga mkono mradi huu ili Serikali ya Tanzania iweze kutimiza malengo ya kuwainua vijana na wanawake kwenye sekta ya kilimo kama ilivyo moja ya agenda kwenye mkutano wa FAO wa mwaka 2023.”

Aidha, Mkurugenzi huyo amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza sekta ya kilimo pamoja na kuboresha mahusiano na mashiriki ya kimataifa, huku akiahidi kutembelea Tanzania mwaka 2024 kwa ajili ya kujionea maendeleo katika sekta ya kilimo, ili kuendelea kuwezesha zaidi sekta ya kilimo na uchumi wa Buluu.

Wakulima, Watumiaji wa Ardhi kusajiliwa Kidijitali
Msimamo ni kuhamasisha ujenzi wa Viwanda - Majaliwa