Mshambuliaji Ranga Chivaviro, aliyekuwa akihusishwa kujiunga na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans kwenye dirisha lililopita la usajili ameueleza Uongozi wa Kaizer Chiefs kuwa anahitaji kuondoka klabuni hapo dirisha lijalo la usajili.

Chivaviro raia wa Afrika Kusini bado ana mkataba wa miaka miwili na Kaizer Chiefs, lakini anahitaji kuondoka klabuni hapo kwa kuuzwa moja kwa moja au kutolewa kwa mkopo, hili limekuja baada ya Mchezaji huyo kukosa nafasi ya kucheza.

Ranga Chivaviro amemueleza wakala wake kumtafutia klabu nyingine ili kukipiga huku akisubiri uamuzi wa Kaizer Chiefs kama watakubali kumuuza au kumtoa kwa mkopo.

Hili suala linasalia kwa Kaizer Chiefs ndio yenye maamuzi kwa Ranga Chivaviro kwa sasa kwa kuwa wana mkataba nae.

Msimu uliopita Chivaviro alikuwa akikimbizana na Fiston Mayele kwenye mbio za ufungaji Bora katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo Mayele akiwa Young Africans alifanikiwa kuwa mfungaji bora kwa mabao 7 huku Chivaviro akishika nafasi ya pili kwa mabao 6.

Aidha, Ranga alitajwa kuwa ndiye angemrithi Mayele baada ya kutimkia Pyramids FC ya Misri lakini mambo yalikwenda ndivyo sivyo kwa Young Africans huku Kaizer wakifanikiwa kumsajili.

Simba yaahidi makubwa African Football League
Wakulima, Watumiaji wa Ardhi kusajiliwa Kidijitali