Beki wa England, Harry Maguire amesema mashabiki waliomzomea kiungo Jordan Henderson sio mashabiki wa nchi hiyo.

Henderson alizomewa alipotolewa katika ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki kati ya England dhidi ya Australia na alipoingia kwenye ushindi wa 3-1 wa kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Italia juzi Jumanne.

Nahodha huyo wa zamani wa Liverpool, Henderson alikosolewa kwa kujiunga na Al-Ettifaq ya Saudi Arabia msimu huu wa joto.

“Mashabiki sahihi wa England hawazomei wachezaji,” alisema Maguire na kuongeza: “Usiwazomee wachezaji wanaojitolea maisha yao kucheza na kufanya kila wawezalo kuifanya nchi hii kuwa na kumbukumbu nzuri na kuwa na wakati maalum kwa ajili yao na familia zao.”

Mo Dewji awalisha sumu wachezaji Simba SC
Mahakama yapigilia msumari ununuzi Kampuni ya Saruji