Serikali Nchini, imesema itaendelea kufanyia maboresho na kutatua changamoto zinazoikabili Shule ya Polisi Tanzania, iliyopo Mkoani Kilimanjaro na kuifanya iwe ya kisasa zaidi.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Mmuya ambaye aliongoza Makatibu Wakuu Wenzake toka Wizara ya Fedha, Maji na umwagiliaji na Ardhi, ameyasema hayo wakati walipotembelea Shule hiyo kwa ajili ya kukagua miundombinu iliyopo na mazingira ya kujifunzia wanafunzi.

Katika Ukaguzi huo wamebaini uwepo wa changamoto kadhaa ambapo baada ya kuzijadili kwa pamoja wameahidi kwenda kuzitafutia majawabu na hatimaye kupelekea mazingira ya Shule hiyo kuwa katika hali ya usasa zaidi.

Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Awadh Juma Haji ameipongeza Serikali kwa namna inavyosaidia kutatua changamoto mbalimbali ndani ya Jeshi hilo.

Wengine waliombatana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ni Prof. Jamal Katundu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, huku Wizara ya Fedha ikiwakilishwa na Renatus Msagira kwa niaba ya Katibu Mkuu ambapo Wizara ya Ardhi iliwakilishwa kwa niaba ya Katibu Mkuu na Alphonce Lekulo.

Chanzo ajali ya Basi iliyouwa 18 chatajwa
Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 22, 2023