Zifuatazo ni baadhi ya nukuu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alizozitoa wakati wa hafla ya utiaji saini Uwekezaji na Uendeshaji wa Sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma Oktoba 22, 2023..

“Nataka niwahakikishie kuwa au niwape uhakika Watanzania wote kwamba maslahi mapana ya nchi yetu yamezingatiwa.”

“Kwa mfano amesema hapa Mkurugenzi hakuna atakayepoyeza kazi. Awe mwajiriwa wa bandari au hata wanaofanya kazi zao bandarini. Hakuna atakayepoteza kazi. Kutakuwa tu na kufuata mfumo fulani katika kufanya kazi zetu ili viwango zile vikae sawa tuendane na Dunia.”

“Kinachofanyika kama nilivyosema ni kuhakikisha bandari inaendeshwa katika viwango vinavyokubalika duniani, kukuza ufanisi na biashara na hatimae kukuza mapato ya nchi yetu,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Samia Suluhu Hassan.

Bandarini kuna changamoto lazima tuzitatue - Serikali
Ushindani wa Bandari: Lazima tuongeze ufanisi - Rais Samia