“Katika mzunguuko wote wa majadiliano, nilichobaini ni kwamba sote Watanzania tunakubaliana kuwa tunayo changamoto pale bandarini.

Tunatofautiana tu juu ya namna ya kuzitatua. Wapo wanaoamini sisi wenyewe bila mbia tungeweza kuzitatua.

Ni mawazo mazuri ya kimapinduzi, lakini yapo mbali na uhalisia. Na njia hiyo itatuchukua muda mrefu sana kufika.

Wakati Dunia inakwenda mbio, sisi tutakua bado tunasota. Na isitoshe tulishajaribu lakini hatukufanikiwa.

Kwa hiyo mikataba hii imezingatia maoni yote yaliyotolewa kwa mtu mmoja mmoja na kupitia makundi ya kijamii pamoja na sheria na taratibu zote za nchi yetu.

Nataka niwahakikishie kuwa maslahi yote mapana ya nchi yamelindwa.”

Nukuu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Bandari kuwatoa umasikini Watanzania - Dkt. Mpango
Dkt. Samia: Niwape uhakika maslahi ya nchi yamelindwa