Kocha Mkuu wa West Ham, David Moyes amedai kuwa uzembe wa wachezaji wake umechangia kwa kiasi kikubwa kichapo cha mabao 4-1 walichopata kutoka kwa Aston Villa ugenini mwishoni mwa juma lililopita (Jumapili – Oktoba 22).

Mabao mawili ya Douglas Luiz na mengine yaliyofungwa na Ollie Watkins na Leon Bailey yalitosha kuiporomosha West Ham hadi nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL) na hivyo kuanza kuweka rehani matumaini ya kumaliza katika nafasi za juu mwishoni mwa msimu.

Moyes amesema hakufurahishwa na kilichofanywa na wachezaji wake ambao walicheza kana kwamba wamelazimishwa.

“Makosa makubwa binafsi wakati mambo hayakutuendea vizuri.

“Tulipoteza fursa nyingi za kufunga mabao na hilo ndilo lililonikwaza.

“Sijawahi kuwa na timu iliyofungwa mabao manne mepesi kama livyokuwa Jumapili,” amebwatuka Moyes.

Waliokatisha masomo kwa ujauzito warejea Shuleni
Madereva magari ya familia chanzo ajali za Barabarani