Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Rebeca Nsemwa amesema kucheleweshwa kwa hati miliki ya Viwanja kwa Wananchi ni sawa na kuwacheleweshea maendeleo, kwani wanashindwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuomba mikopo kwenye mabenki na kufanya maendeleo kwenye maeneo yao.

Nsemwa ameyasema hayo wakati akizindua wiki ya Kliniki ya Ardhi Manispaa ya Morogoro, na kudai kuwa Ardhi ni rasimali muhimu na uwepo wa mgororo au kutokuwa na hati ya ardhi haiwezeshi kuwa salama na ni rahisi watu kuvamia eneo la mmiliki halali.

Amesema, anaipongeza timu ya Makamishina wa Ardhi Manispaa ya Morogoro kwa kuwakutanisha Wananchi na kutatua kero za ardhi zilizodumu kwa muda mrefu, kwani Mwananchi hatakua na uwezo wa kusikilizwa kero yake na kutatuliwa kwa wakati

Awali, Kamishna wa Ardhi mkoa wa Morogoro, Frank Minzikuntwe alisema yeye na timu yake wamekubaliana kutoa suluhu kwa Wananchi, kwani timu ya Makamishina wa Ardhi Manispaa ya Morogoro itagawa hati kwa Wananchi watakaoomba na kulipia itashughulikiwa muda huo.

Man City, Liverpool zagongana kwa Musiala
Waandishi elimisheni Umma matokeo ya Sensa - RC Mongela