Ollie Watkins amekiri kuwa lengo lake ni kujumuishwa katika kikosi cha England kitakachoshiriki Euro 2024 baada ya kufunga tena Aston Villa ikishinda mabao 4-1 dhidi ya West Ham.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alitengeneza bao la kwanza la Douglas Luiz na kutikisa nyavu kwa mguu wa kushoto huku kikosi cha Unai Emery kikipanda hadi nafasi ya tano kwenye Ligi ya England.

Baada ya kufikisha jumla ya mabao nane katika michuano yote msimu huu, Watkins amepania kung’ara akiwa na ‘Simba Watatu’ kwenye michuano itakayofanyika chini Ujerumani.

Alisema: “Zaidi ya mabao 20 na kwenda kwenye michuano ya Euro ndicho ninachotaka kufanya. Hayo ndiyo malengo yangu na ndicho ninachokipigania.

“Najua kiwango cha klabu yangu lazima kiwe kizuri nikiwa na Villa.”

Juu ya kiwango chake tangu Emery kuwasili, Watkins aliongeza: “Kabla nilikuwa nakimbia kwenye bendera za pembeni na kukimbizana na mambo, lakini sasa tuna mabeki wa pembeni wanaofanya hivyo hivyo, najaribu kukaa kati. Ninafanya mbio za ujanja zaidi, naweza kusema.

“Kuna wakati nilikuwa nikishuka sana ili kupata kugusa mpira wakati sasa sijasumbuka na hilo.

Aziz Ki ashindwa kuchagua bao bora
Wahimizwa usimamizi kuhimili athari mabadiliko Tabianchi