Mkurugenzi wa Real Madrid, Jose Angel Sanchez, amekanusha ripoti kwamba Luka Modric anaweza kuondoka kuelekea Saudi Arabia mwezi Januari 2024.

Modric amekiri wazi kutofurahia dakika chache alizocheza msimu huu, akiwa ameanza mechi tatu pekee za La Liga.

Jumla ya dakika 414 za Modric katika mashindano yote ni chini ya wachezaji wengine 14 na inazidi jumla ya Ferland Mendy, Lucas Vazquez, Andriy Lunin, Brahim Diaz na majeruhi Eder Militao.

Ni kwa sababu hiyo ndipo tetesi za kuondoka kwa Modric Januari 2024 zimeibuka na Saudi Arabia imetajwa kuwa huenda ikafikiwa, ingawa Sanchez amekanusha uvumi huo.

“Hakuna mazungumzo rasmi kwa upande wa maafisa wa Ligi ya Saudia kumjumuisha Luka Januari 2024, na hatuna maoni yoyote juu ya kuondoka kwake kwenye timu kwa sasa,” Sanchez aliiambia Al-Riyadiyah.

Ripoti kutoka nchini Hispania hivi majuzi zilidai kuwa Kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti amewakasirisha wasimamizi wa klabu hiyo kwa kumpanga Modric pamoja na mkongwe mwenzake Toni Kroos kutafuta mshindi dhidi ya Sevilla Jumamosi (Oktoba 21).

Modric na Kroos waliwahi kuwa safu muhimu ya kiungo ya Santiago Bernabeu, lakini wote wameshuka chini ya Ancelotti, ambaye ameshuhudia Madrid ikiweka akiba ya baadhi ya wachezaji makinda wa kati wa mchezo huo.

Federico Valverde, Aurelien Tchouameni na Eduardo Camavinga wote wameibuka nyota, huku kumnunua Jude Bellingham majira ya joto kukiibua mabadiliko ya kimbinu yaliyowaacha Modric na Kroos wakipigania mustakabali wao.

Modric amekataa kuondoa uwezakano wa kuondoka katika klabu hiyo Januari iwapo ataendelea kutatizika kwa dakika, huku waajiri wa zamani Dinamo Zagreb wakitarajia kuungana naye tena.

Ngoma awapoteza Mzamiru, Kanoute
Aziz Ki ashindwa kuchagua bao bora