Kufuatia utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009, kiasi cha manunuzi ya bidhaa za ndani ya nchi katika miradi mikubwa ya madini, kimeongezeka kutoka Dola za Marekani Bilioni 700 kwa mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani trilioni kwa mwaka 2022.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam hii leo Oktoba 25, 2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali katika Mkutano wa Madini na Uwekezaji Tanzania 2023 na kuongeza kuwa mafanikio hayo yamechochea sekta ya madini kukua kutoka asilimia 9.4 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 10.9 mwaka 2022.

Amesema, “thamani ya madini yanayosafirishwa nje ya nchi kutoka Dola za Marekani bilioni 3.1 kwa mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 3.4 kwa mwaka 2022. Pili, kuongezeka kwa ajira katika miradi mikubwa ya madini kutoka ajira 14,308 mwaka 2021 hadi ajira 16,462 mwaka 2022.”

Mkutano huo, umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali Nchini, Viongozi na wawakilishi wa Serikali za nchi mbalimbali duniani, Viongozi wa dini, Viongozi na wawakilishi wa Taasisi binafsi na Kampuni mbalimbali za uwekezaji za ndani na nje ya nchi, Wafanyabiashara, Wataalamu na Wadau wa Sekta ya Madini.

Eric Dier kuvutwa Allianz Arena
Ngoma awapoteza Mzamiru, Kanoute