Mtendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Same, Koplo Sure Amos amewataka Wanafunzi wa Shule ya Msingi Majengo ya Wilayani humo, kutambua mabadiliko ya nyakati hivyo wawe makini na sehemu wanazopendelea kucheza ili kuendelea kuwa usalama.

Koplo Sure ameyasema hayo wakati akizungumza na Wanafunzi hao Mkoani Kilimanjaro na kuongeza kuwa wanatakiwa kutocheza katika mazingira hatarishi kwa lengo la kuepuka kufanyiwa vitendo vya kihalifu ikiwemo ukatili wa kijinsia.

Amesema, “hampaswi kucheza kwenye mazingira hatarishi ambayo yanaweza kupelekea matukio kama ya ubakaji, ulawiti kwenu, badala yake mnapomaliza masomo mnapaswa kuelekea nyumbani moja kwa moja kwani nyakati zimebadilika mnahitaji kuwa makini mnapoona viashiria vya uhalifu.”

Aidha, Koplo Sure pia amewaonya Baadhi ya Wanafunzi wenye tabia ya kupitia maeneo hatarishi wanapotoka shuleni, ambapo amewataka kuacha tabia hizo zisizokua njema kwa jamii na kuwatapa kuacha uoga wa kutoa taarifa za matukio ya ukatili na badala yake kila mmoja anatakiwa kuwa mlinzi kwa mwenzake.

Sekta ya Madini nguzo muhimu uchumi wa Taifa - Dkt. Biteko
Benchi kumkimbiza Thomas Partey