Nyota wa Singida Big Stars, Duke Abuya amesema ni muda kwao wa kuonyesha ubora wao mbele ya Young Africans ambayo imekuwa ikipata matokeo dhidi ya kikosi chao tangu kilipopanda Ligi Kuu.
Singida Big Stars itakua mgani wa Young Africans baadae leo Ijumaa (Oktoba 27), katrika mchezo wa mzunguuko wasabi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Duke aliyesajiliwa akitokea Police FC ya Kenya aliongeza ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC katika mchezo uliopita, umewaongezea morali kubwa huku akianisha licha tu ya kuiheshimu Young Africans kutokana na ubora wao ila hawatoingia kinyonge.
“Kila mchezo ni mgumu kama iliyopita na sisi wachezaji jukumu letu ni kuhakikisha tunapambana kwa ajili ya timu, hii ni nafasi nyingine ya kuonyesha ukubwa tuliokuwa nao kwa sababu uwezo na uzoefu tunao wa kukabiliana na yeyote,” alisema.
“Tunaiheshimu Young Africans ila hatotakuja kinyonge kwani tunahitaji kupata pointi tatu pia,” amesema.
Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na alama 15 sawa na Simba SC, lakini ina mchezo mmoja zaidi, huku Singida Big Stars ikifikisha alama 08 zinazoiweka kwenye nafasi ya tisa.