Klabu ya AC Milan huenda ikachukuliwa hatua za kisheria na Newcastle United baada ya kuwauzia Sandro Tonali ambaye ameathirika na michezo ya kamari kwa mujibu wa ripoti.
Tonali endapo atapatika na na hatia atafungiwa miezi 10 kujihusisha na masuala ya michezo hivyo Newcastle itapata pigo.
Kiungo huyo wa kati aliyenunuliwa kwa Pauni 55 Milioni alijumuishwa dhidi ya Borussia Dortmund akitokea benchi juzi Jumatano (Oktoba 25) usiku licha ya kukabiliwa na kesi hiyo na kuambulia kichapo cha abao I-0.
Lakini huenda hiyo ikawa mechi yake ya mwisho hadi msimu ujao baada ya kukubali alijihusisha na michezo ya Kamari wakati anakipiga AC Milan.
Pia Tonali mwenye umri wa miaka 23 amekubali kufanyiwa matibabu na kuunga mkono kampeni za kupinga kamari hususan kwa wachezaji.
Kwa upande Newcastle iliapa itafanya uchunguzi kwa kufuata sheria zote kufuatia sakata hilo la nyota huyo wa kimataifa wa Italia na AC Milan.
Na ripoti za Italia zinadai mshahara wa Tonali wa Pauni 7 milioni unaweza kusikitishwa.
Maswali yamebaki kuulizwa ni kweli AC Milan ilifahamu Tonali alikuwa anachunguzwa na mamlaka ya kuzuia Kamari kwa wachezaji kabla ya kumuuza Newcastle? Majibu ni kwamba tusubiri tuone.
Tonali atakosa mechi zilizobaki za kufuzu Euro 2024, lakini anatarajiwa kuruhusiwa kufanya mazoezi na Newcastle.