Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amewataka wataka Wananchi kuachana na matumizi ya fedha taslimu na badala yake kuhamia kwenye matumizi ya kidijitali, njia ambayo ni salama na itakayowaepusha na tatizo upotevu wa pesa, huku akiipongeza Benki ya NMB kwa kuchangia maendeleo kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo za Afya na elimu.

Kindamba ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya NMB ya Mastabata Halipoi, iliyofanyika mkoani Tanga na kusema hatua hiyo inaunga mkono jitihada za Serikali katika kuwafikia Wananchi na kwamba usalama wa fedha kwa sasa ni muhimu kwani unaepusha mambo mengi ikiwemo matumizi yasiyo ya lazima.

Amesema, “kuendelea kuchangia Uchumi unaokwenda kidigital ni pamoja na kuachana na matumizi ya fedha taslimu, mbali na usalama wa fedha zako ni bora zaidi kutumia matumizi ya kadi kwa sababu kama nchi tunaingia gharama kubwa kuchapisha fedha, kwahiyo matumizi ya fedha kupitia mitandao ni salama zaidi kwa ajili ya malipo.”

Awali Mkuu wa kitengo cha Kadi kutoka NMB, Filbert Casmir alisema wametenga Shilingi 350 Million ambazo zitakazotolewa kila wiki kwa wateja 100, atakayepatiwa kitita cha shilingi 100, 000 na endapo mteja atakutwa na mtoa huduma akifanya malipo ya bidhaa kupitia kadi yake ya Benki atazawadiwa Shilingi 50, 000, papo hapo.

“Tunaendelea kuhamasisha malipo kwa kutumia kadi na kuachana na matumizi ya fedha taslimu,  kupitia kampeni hii tutakuwa na droo ya kila wiki na tumeandaa kiasi cha shilingi million 350 ambazo zitakuwa zikishindaniwa kwa wateja wetu washindi 100, kila mmoja atashinda pesa taslimu laki 1 lakini tukikukuta unafanya manunuzi kupitia kadi palepale tukupatia shilingi elfu hamsini.” 

Mbali na washindi hao watakaozawadiwa kila wiki, pia kutakuwepo na droo ya kila mwezi kila mshindi akiingiziwa Shilingi 500,000 kwenye akaunti yake na kupewa ofa ya kwenda kutalii Zanzibar sambamba na zawadi ya pamoja kwa washindi 7 na wenza wao, watakaogharamikiwa safari ya kwenda Afrika Kusini kwa muda wa siku tano, wakilipiwa kila kitu na NMB.

Gamondi amekataa kutoka kileleni Ligi Kuu
Pawasa ampongeza Kibu Denis kwa nidhamu