Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amewataka mawaziri wa wizara zinazohusika na michezo Zanzibar na Tanzania Bara kushirikiara pamoja na kujipanga ili kuona namna bora ya utoaji huduma wakati wa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027).

Akizungumzia mjini Unguja baada ya kushiriki mashindano ya Tigo-Zantel Zanzibar International Marathon, Rais Mwinyi alisema hiyo ni fursa nzuri ya pamoja, ambayo hawapaswi kuipoteza.

Alisema kuwa katika mashindano hayo kutakuwa na mambo mengi yatajitokeza yenye faida kwa nchi, hivyo ni lazima wajipange ili wasipoteze fursa hiyo.

Alisema kila mtu kwa upande wake aone kuwa hiyo ni fursa kubwa inayokuja, na wajipange ili waweze kutoa huduma bora na kunufaika na michezo hiyo mikubwa ambayo inakuja nchini mwetu.

Rais Mwinyi aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapa na wao nafasi ya kuwa moja ya vituo, ambavyo michezo hiyo itachezwa.

Aidha alisema kuwa michezo ina umuhimu wake wa kipekee, kwani mbali na kuleta utalii, lakini pia imekuwa ikileta afya.

Alisema wakiwa na tabia ya kufanya mazoezi yatawaondolea au kupunguza kwa kiasi kikubwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kuwasihi wananchi wafanye mazoezi kila wakati kwa kuunda vikundi mbalimbali ili vishiriki mazoezi.

Ukitembea kilometa tano kwa siku hata isifike itakujenga vizuri afya yako, kwa hiyo nimefurahi sana kuwa miongoni mwa washiriki wa marathoni hii ambayo ina faida kubwa sana ikiwemno kujenga afya na kupata watu wenye vipaji ili kupata ajira”, alisema.

Waziri Utamaduni, Sanaa na Michezo Tanzania, Dk Damas Ndumbaro na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, walisema kuwa wamekuwa na ushirikiano wa kutosha katika sekta mbazo wanazisimamia.

Walisema kuwa kwa kipindi kifupi ambacho wamekutana  wameshafanya vikao vingi vya mashirikiano baina yao kuona kwa namna gani wataendeleza sekta hiyo ya michezo kwa pande zote mbili.

TPBRC yawapongeza Ibrah Class, Majiha, Mpenda
Robertinho atoa pongezi, aigeukia Young Africans