Viongozi muhimu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzoua, wamezua hofu kikosini hapo kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC.

Aziz Ki na Pacome, wamezua hofu baada ya taarifa kutoka walipata maumivu katika mchezo uliopita dhidi ya Singida Fountain Gate ambao Young Africans ilishinda 2-0.

Jumapili (Novemba 05), Young Africans itapambana na Simba SC katika mchezo wa Kariakoo Dabi uliopangwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es salaam.

Daktari wa Young Africans, Moses Etutu, amesema: “Pacome aligongana na mchezaj wa Singida na kupata maumivu ya goti, lakini baada ya kupata dawa za kutuliza maumivu amekuwa sawa.

“Aziz Ki aliumia sehemu ya chini ya mguu, tunatarajja kumfanyia vipimo zaid ili kupata taarifa kamili ya ukubwa wa jeraha lake.

Ikumbukwe kuwa, wachezaji hao katka mchezo dhidi ya Singida, wote walitolewa kipindi cha pili, Pacome alianza kumpisha Skudu Makudubela, kisha Aziz Ki akatoka na kuingia Clement Mzize.

Mama wa Luis Diaz apatikana Colombia
Eddie Nketiah dhahabu inayong'aa Arsenal