Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema anaamini kuwa ukifanyika ukaguzi mwingine wa usalama wa anga wa Mataifa barani Afrika, Tanzania itafikisha alama zaidi ya 90 na kuwa nafasi za juu tofauti na ilivyo sasa.
Mbarawa ameyasema hayo hii leo Oktoba 30, 2023wakati akifungua maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Amesema, “Serikali inaendelea na ufungaji wa mitambo ya kuongoza ndege kwenye viwanja vya ndege vilivyoko Pemba, KIA, Mwanza, Songwe na Arusha. Ninaamini sekta hii itapiga hatua kwa kasi zaidi katika kipindi kifupi kijacho.â
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania – TCAA, Hamza Johari alisema taasisi hiyo ilianzishwa rasmi Novemba Mosi, 2003 na inatoa huduma za uongozaji ndege katika viwanja 15 hapa nchini.
Amevitaja viwanja hivyo kuwa ni Arusha, Geita, Dodoma, Kigoma, Mtwara, Mwanza, Zanzibar, Pemba, Dar es Salaam, Songea, Songwe, Iringa, Tanga, Tabora na Bukoba ambako hivi karibuni wamefunga mitambo ya kuongoza marubani wakati wa hali mbaya ya hewa.