Uongozi wa Klabu ya AS Roma umedhamiria kufanya mabadilishano na Klabu ya Chelsea kwa kuwapa Tammy Abraham mwenye umri wa miaka 26, ili kumsainisha mkataba wa kudumu Romelu Lukaku wakati wa dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

AS Roma inahitaji kumsainisha mkataba wa kudumu Lukaku kwa sababu imevutiwa na kiwango chake tangu ajiunge nao katika dirisha lililopita.

Ripoti zinadai Abraham anataka kuondoka mwisho wa msimu huu wakati ambao kocha Jose Mourinho pia anatarajiwa kuondoka na ripoti zikimhusisha na kuwa kwenye mpango wa kutimkia nchini Hispania, England na Saudi Arabia.

Tammy mwenyewe anadaiwa kutamani kuondoka ili kubadilisha mazingira na kupata changamoto mpya baada ya kutofanya vizuri msimu uliopita na alifunga mabao tisa tu tofauti na msimu wake wa kwanza alifunga mabao 27 kwenye mechi 53.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England tangu uanze msimu huu hajacheza mechi hata moja kutokana na majeraha ya goti yanayomwandama ambayo anatarajiwa kupona mwakani. Mkataba wake unatarakiwa kumalizika mwaka 2026.

Arsene Wenger aichambua Man Utd
Utaratibu wa mila za Makabila unaoshangaza wengi Afrika