Kiungo wa FC Barcelona lkay Gundogan amefichua siri kwamba baadhi ya wachezaji wenzake hawakuumizwa na kichapo dhidi Real Madrid kwenye mechi ya El Classico uliochezwa Jumamosi (Oktoba 28).

Kiungo huyo alitamani kuona wenzake wakihuzunika katika vyumba vya kubadilishia nguo kufuatia kichapo cha mabao 2-1 ambayo yote yalifungwa na Jude Bellingham.

Gundogan ndiye aliyefunga bao la kuongoza kwa upande wa FC Barcelona kabla ya Bellingham kufunga mabao mawili na kuipa ushindi Madrid.

Kutokana na kichapo hicho FC Barcelona imeshuka nafasi ya tatu ikiwa nyuma kwa pointi nne dhidi ya Madrid na Girona kwenye msimamo wa La Liga.

Gündogan alifichua siri kwamba: “Baada ya matokeo mabaya nilitarajia kuona hasira za wachezaji wenzangu ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo.

“Ndio watu wamesikitika baada ya mechi hiyo kubwa, na matokeo kwa ujumla, nilitamani kuona hasira zaidi lakini hakuna kabisa. Unajua unaweza ukafanya vizuri katika mambo fulani lakini ukanyamaza.”

FC Barcelona ilipoteza pointi tatu katika mechi tano za mwisho za La Liga baada ya kutoa sare dhidi ya Mallorca na Granada.

Pia, Ilianza msimu bila kufunga bao dhidi ya Getafe, na Gundogan amekiri kwamba timu inahitaji kuimarika zaidi ili kuwa ushindani.

“Tunatakiwa kupambana kwa sababu Real Madrid au Girona wana kasi, sikuja hapa kwa ajili ya kupoteza mechi dhidi ya timu kama hizi au kutengeneza uwiano kuwa mkubwa kwenye msimamo, aliongeza nyota huyo wa zamani wa Man City.

Serikali yaanza mapitio sera ya Taifa Watu wenye Ulemavu
Utawala Bora: Ujerumani yafurahishwa na kasi ya Rais Samia