Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini Tottenham Hotspurs italeta ushindani katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu 2023/24.

Spurs ambayo imezaliwa upya chini ya kocha mpya Ange Postecoglou imejikita kileleni kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 10.

Ushindi wa ljumaa (Oktoba 27) dhidi ya Crystal Palace unaiacha klabu hiyo ya London kwa pointi mbili mbele ya mahasimu wao, Arsenal kwa kushinda mara nane na kutoka sare mara mbili kwenye Ligi Kuu msimu huu.

Siku zote napenda kusema kile ninachohisi,” Wenger amesema kupitia beIN Sports.

“Kwa undani, ninaamini Tottenham itakuwa moja kati ya timu inayogombea ubingwa wa ligi msimu huu. Walimnunua James Maddison, ambaye ni mchezaji mzuri. Yeye ndiye kiungo wa kutokea chini hadi kiungo cha juu na aliongeza ubunifu wa kiufundi kwenye timu.

“Pia, walimnunua Micky Van de Ven, ambaye namuona ni mchezaji wa kipekee kabisa. Walikuwa na udhaifu kwenye nafasi ya kipa kwani msimu uliopita kipa Hugo Lloris hakuwa na misimu bora. Na kiwango chao kuanzia kati kwenye safu ya kiungo ipo vizuri kwa sasa,” alisema Wenger.

Hata hivyo, Wenger anaamini timu kadhaa pia zipo katika kinyang’anyiro cha kuwani ubingwa msimu huu:

“Msimu huu naweza kuitaja Arsenal kwa ajili yangu, Liverpool, Tottenham, Manchester City bila shaka wapo kwenye msafara huo,” ameongeza.

Arsenal, Liverpool ziliibuka na ushindi kwenye mechi zao mwishoni mwa juma lililopita, huku Manchester City ikiichapa Manchester United mabao 3-0.

Arsenal ilibamiza Sheffield United mabao 5-0, Liverpool ikiondoka na ushindi wa mabao 3-0 ilipomenyana dhidi ya Nottingham Forest.

Elimu kwa Umma: Polisi, Wanahabari Manyara kushirikiana
Mkataba wa IRENA: Bunge laridhia wasilisho la Dkt. Biteko