Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, ambaye yupo Nchini kwa ziara ya siku tatu.

Dkt. Samia amezungumza na Rais Steinmeier Ikulu jijini Dar es Salaam hii leo Oktoba 31, 2023 juu ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii baina ya mataifa haya mawili.

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023. Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mbele ya Mkutano na Waandishi wa Habari, Rais Samia alisema uhusiano baina ya Tanzania na Ujerumani unafikia miaka 60 sasa, ambapo ndani ya kipindi chote wamekuwa rafiki wema.

Mbali na Tanzania kuishukuru Ujerumani kwa kuchangia kwenye miradi kadhaa ya maendeleo, Rais Steimeier alisema amefurahishwa na kasi ya Rais Samia ya kujenga nchi katika mfumo wa utawala bora na wa kisheria.

Wachezaji FC Barcelona wamshangaza Gundogan
Gunia la Mpunga lasababisha mauaji Mwanza