Lydia Mollel – Morogoro.

Mbunge wa Morogoro Mjini, Dkt. Abdulaziz Abood amesema zaidi ya shilingi 100 milioni zimetuka kukamilisha miradi mbalimbali katika Mkoa wa Morogoro.

Abood ameyasema hayo baada ya kufanya ziara ya siku mbili na kutembelea kata tisa kukagua miradi hiyo ya maendeleo.

Mbunge wa Morogoro Mjini, Dkt. Abdulaziz Abood.

Amesema, fedha hizo zimetumika kuamarisha miradi ya Afya na elimu, huku akitoa Vifaa Tiba na kukamilisha Majengo ya Hospitali, Madarasa na Vyoo vya Shule.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya Wananchi wa jimbo hilo wamepongeza juhudi xa kuimarisha upatikanaji wa maendeleo, huku wakitaka kuwekwa mkazo zaidi wa kuimarisha huduma za Sekta ya Afya na Maji.

Wakenya wamtaka Mfalme Charles III kuomba radhi
Balozi Mbarouk ampongeza Dkt. Tulia Urais IPU