Mwanamke mmoja Salma Abdallah (37), Mkazi wa Lumala ya Wilayani Ilemela amesomewa shitaka la kujihusisha na matumizi ya Dawa za Kulevya aina ya Bangi, katika Mahakama ya Wilaya hiyo iliyopo Mkoani Mwanza.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Amani Sumari Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Monika Mweli alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Oktoba 1 – 10, 2023, eneo la Lumala la Wilayani Ilemela.

Hata hivyo, Salma alikana shitaka hilo na kurejeshwa rumande kwa kutokidhi masharti ya dhamana ya kutakiwa kuwa na wadhamini wawili, kwa kila mmoja kusaini bondi ya maneno ya Shilingi Milioni 2, Kitambulisho na Barua ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.

Salma Abdallah, anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na Kifungu namba 17 (1) (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Sura ya 95 toleo la Mwaka 2019, ambapo shauri hilo limeahirishwa hadi Novemba 11, 2023 litakaposomwa tena.

Aishi Manula aipasua Simba SC
Mashabiki Chelsea waingia hofu EPL