Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo ameipongeza Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira – NEMC, kwa utekelezaji wa majukumu yake.

Jafo ametoa pongezi wakati akizungumza kwenye kikao cha 16 cha Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya NEMC kilichofanyika jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao cha 16 cha Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya NEMC.

Amesifu utaratibu wa kutembelea maeneo mbalimbali kukagua shughuli za kulinda mazingira hususan katika migodi iliyopo ya mkoani Geita na kwengineko.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakati wa kikao cha pamoja na Menejimenti ya Baraza hilo kilichofanyika jijini Dodoma.

Aidha, ametoa rai kwa Bodi hiyo kuendelea kuisimamia NEMC inapotekeleza Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 katika maeneo mbalimbali na kuwachukulia hatua wanaoikiuka.

Jafo amesema ni jukumu la NEMC kuhakikisha wenye viwanda, migodi na maeneo ya starehe yanafuata sheria ili kudhibiti changamoto za uchafuzi wa mazingira zikiwemo utiririshaji wa majitaka, moshi au kelele na mitetemo.

Naj Razi azitega Arsenal, Chelsea, Real Madrid
Upigaji wamfikisha Mahakamani mshauri wa Kodi