Shirika la umeme Nchini – TANESCO, linatarajia kujenga kituo kidogo cha umeme (Switching Station), Wilaya ya Ushetu eneo la Nyamirangano, ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakati akijibu swali la Mbunge wa Ushetu, Emanuel Peter Cherehani aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kupeleka umeme wa uhakika katika Halmashauri za Ushetu, Msalala, na Kahama.

Akijibu swali hilo, Kapinga amesema TANESCO pia itaongeza njia nyingine za umeme kutokea kituo hicho kwenda Ushetu, Msalala, na Kahama, ikilenga kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo.

Amesema, ujenzi wa mradi huo unatarajia kuagharimu kiasi cha Shilingi 12 Bilioni na mradi unategemewa kukamilika katika Mwaka wa Fedha wa 2024/2025.

TAMWA-ZNZ yatangaza Tuzo Habari za Wanawake, Uongozi
Brentford yapandisha ada ya Ivan Toney