Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Babati Vijiji, John Noya ameliagiza shirikishi la umeme Tanesco Mkoani Manyara kuhakikisha wanasambaza umeme Katika Shule za msingi na Sekondari zilizopo Katika Halmashauri hiyo, huku Nadiwani wakitaka Watendaji wa Shirika hilo kuwa wakweli kwa Wananchi.

Agizo hilo, limetolewa mbele ya Mtaalamu kutoka Tanesco Mkoa wakati akiwasilisha hoja za Shirika hilo la umeme, kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri kilichofanyika Novemba 2, 2023 Katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Babati vijijni.

Amesema, ni jambo la kushangaza kuona Shule za Msingi na Sekondari hazina Miundombinu ya Umeme Katika Halmashauri hiyo, kwani uwepo wa umeme mashuleni husaidia kuongeza utendaji kazi kuwa wa kisasa kwa Walimu pamoja na Wanafunzi kujisomea.

Kwa upande wao baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Babati vijijini, wameiomba Tanesco Mkoa wa Manyara kujitahidi kuwa wakweli wakati wa kusambaza umeme katika kata mbalimbali za Halmashauri hiyo na kuacha kauli za udanganyifu Kwa wananchi.

Naye Mhandisi Manumbu Sabi, ambaye ni Kaimu Muhandisi mipango TANESCO Manyara amewaomba Madiwani pamoja na Baraza wajitahidi kuhakikisha wanatoa ushirikiano wakati wa zoezi la kusambaza Umeme Katika maeneo yote yaliyopo kwenye Mpango kwenye Halmashauri hiyo.

Kocha Bakari Shime aigeukia Togo
Charahani aihoji Serikali mkakati wa Umeme