Umoja wa Mataifa – UN, kitendo cha hali ya hewa na mamlaka za Afya umesema mabadiliko ya tabia nchi yameleta tishio la afya kutokana na ongezeko la majanga ya hali ya hewa na joto la kupindukia.

Kupitia ripoti ya kila mwaka ya hali ya hewa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa – WMO, linataka kuwepo kwa mifumo bora ya kutoa tahadhari inayoweza kujumuishwa katika sera ya afya ya umma.

WMO inasema taarifa kuhusiana na hali ya hewa hazijumuishwi kikamilifu katika mipango ya huduma ya afya na kwamba kati ya mwaka 2000 na 2019 vifo vilivyosababishwa na joto vinakadiriwa vilikuwa 489,000 kwa mwaka. 

Shirika hilo linasema joto la kupindukia ni chanzo kikubwa cha vifo vinavyotokana na hali mbaya ya hewa, ila katika nchi zilizoathirika na kadhia hiyo, ni nusu tu ya wanaofanya maamuzi kuhusiana na masuala ya afya ndio wenye uwezo wa kupata huduma za tahadhari.

Mawaziri wa Afrika wakutana Johannesburg
Msako Wanachuo wahalifu, watovu wa maadili waanza