Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta amesema amekerwa na kiwango cha timu yake kilichosababisha kuondolewa katika michuano ya Kombe la Ligi ‘Carabao Cup’.

Arsenal juzi Jumatano (Novemba Mosi) ilikubali kichapo cha mabao 3-1 katika mchezo wa raundi ya nne ya michuano ya Kombe la Carabao, uliofanyika jijini London, England.

Kocha Arteta alifanya mabadiliko ya wachezaji sita katika kikosi chake cha kwanza huku mastaa Declan Rice, Bukayo Saka na nahodha Martin Odegaard wakianzia benchi.

Kocha Arteta alisema amechukuzwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake na kusababisha timu hiyo kuondoshwa katika michuano.

“Nimekasirishwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kiwango cha hali ya chini kilichoonyeshwa na wachezaji wa timu yangu.

“Tumeondolewa kuendelea na michuano ya Kombe la Carabao kwani mipango yetu ilikuwa kufika mbali zaidi.

“Baada ya bao la kwanza tulionekana kupoteza mwelekeo kitu ambacho siyo kawaida yetu, nina maumivu makubwa kufuatia kupoteza mchezo muhimu kwetu.

“Tunakwenda kujipanga kuhakikisha tunarejea katika ubora wetu na kufanya vizuri mechi inayofuata ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Newcastle keshokutwa Jumapili,” alisema Kocha Arteta.

Ahmed Ally: Tunakwenda kupiga kwenye mshono
Dilunga nje miezi mitatu