Scolastica Msewa, Kibiti – Pwani.

Chama kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa mkoa wa Pwani – CORECU, kimezindua mnada wa korosho wa mwaka 2023/24 kwa kuuza tani 3854 kwa bei ya shilingi 2094.46 ambapo tani zaidi ya 20,000 za Korosho zinatarajiwa kuuzwa katika mkoa mzima wa Pwani .

Akitangaza bei ya Korosho kwenye mnada huo wa uzinduzi uliofanyika Wilayani Kibiti Mkoani Pwani, Meneja Mkoa wa CORECU Pwani, Mantawela Hamisi amewataka Wakulima kukausha korosho zao, ili ziwe na ubora kwa lengo la kuuza kwa bei nzuri sokoni.

Amesema, Kama Korosho hizo zitakaushwa vizuri hata katika mnada huo wa uzinduzi wangeuziuza kwa bei kubwa zaidi ya walivyouza kwa bei ya shilingi 2094.46 kwa kilo, huku Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo akiwa mgeni rasmi kumuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge.

Kanali Kolombo amewataka wakulima kuzuia utoroshaji wa zao hilo kwenda kuuza katika mikoa jirani na kukosesha mkoa wa Pwani na halmashauri zake mapato huku pia akivitaka vyama vya msingi kuwasaidia wakulima wanaopeleka korosho zao kwenye maghala kuchambua na kuhakikisha wakulima wamekausha vizuri korosho zao.

Amesema, “Vyama vya msingi wasipokee korosho mbichi pale, mkulima yeye anachotaka ni kuuza korosho zake hivyo mwelekeze vizuri mkulima ajue namna ya kuziandaa vizuri ili auze korosho zae zikiwa zimekauka zikubalike sokoni na zinunulike vizuri.”

Manchester United yajisogeza kwa Sacha Boey
Polisi Katavi wabaini uhalifu wa Bajaji