Serikali ya Nchi ya Rwanda, imetangaza kuwa itawaruhusu Waafrika wote kusafiri na kuingia katika Taifa hilo bila visa, hatua ambayo inalenga kukuza usafiri huru wa Watu na Biashara, kama ilivyo katika kanda ya Schengen barani UIaya.

Rais wa Nchi hiyo, Paul Kagame ametoa tangazo hilo katika mji mkuu wa Rwanda Kigali, ambako aliuelezea uwezo wa Afrika kama kivutio cha pamoja cha utalii, licha ya kutegemea asilimia 60 ya watalii wake kutoka nje ya Afrika.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Hatua hiyo, itakapoanza kutekelezwa itaifanya Rwanda kuwa ni nchi ya nne ya Kiafrika kuondoa masharti ya kusafiri kwa Waafrika kwani Nchi nyingine zilizotoa visa kwa raia wa Kiafrika ni Gambia, Benin na Ushelisheli.

Katika hatua nyingine Rais wa Kenya, William Ruto naye alitangaza mipango ya kuwaruhusu Waafrika wote kusafiri bila visa kwenda katika taifa hilo la Afrika Mashariki ifikapo Desemba 31, 2023.

Zanzibar yajipanga fursa Utalii wa Mikutano
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 4, 2023