Serikali Nchini, imeshauriwa kubadili mfumo wa elimu ya Msingi na Sekondari ili kuwaandaa Vijana kupambana na majukumu ya kifamilia wakiwa bado wana nguvu.
Ushauri huo, umetolewa na Mkurugenzi wa Kijiji cha Nyuki na mdau wa elimu, Philemon Kiemi wakati kizungumza kwenye mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Elimu ya Sekondari kwa watu wazima chini ya mradi wa kuboresha elimu ya sekondari SEQUIP.
Amesema, Vijana wengi waliohitimu elimu ya juu nchini wamehitimu wakiwa na umri mkubwa na hivyo kushindwa kupambana na uhalisia wa maisha na kujikuta katikia hali ngumu ya kufanikisha uchumi wa maisha yao na familia kiujumla.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Unyanga na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Geofrey Mdama amewatakia heri katika mitihani yao ya Taifa wanayotarajia kuifanya hivi karibuni.
Awali akisoma risala kwa niaba ya Wanafunzi, Wamilika Richard amesema wanamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa nafasi ya kuendelea na masomo bure baada ya kukatisha masomo yao kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ujauzito.